Wednesday, March 25, 2015

THAMANI MJENGO WA DIAMOND BALAA.


Mwonekano wa Nje Mjengo wa Nyumba ya Diamond.





KUKAMILIKA kwa mjengo wa Staa wa Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ndiyo habari ya mjini kwa sasa ambapo gumzo zaidi ni kuhusu gharama halisi huku mkandarasi mmoja akikisia kuwa si chini ya sh. mil. 400, Risasi Mchanganyiko linakupa stori kamili.

Mjengo huo wa Diamond uliopo maeneo ya Madale nje kidogo ya Jiji la Dar, unadaiwa kufikisha thamani hiyo kutokana na kuwa na vyumba vinne vya kulala, bwawa maalum la kuogelea (swimming pool), sehemu ya mazoezi (Gym), jakuzi, kaunta ya vinywaji, ukumbi wa kuchezea, studio ya muziki, uwanja wa mpira wa kikapu na sehemu ya kuchezea mchezo wa mishale (Darts).

Kwa mujibu wa Diamond, nakshi za dhahabu alizoziweka katika kuta za bafu na chooni pekee, zimemgharimu sh. mil. 70 kitu kinachoendana na utabiri wa mkandarasi huyo kuwa nyumba hiyo inafikia thamani ya zaidi ya sh. mil. 400.

Akiuzungumzia mjengo huo baada ya kuuona, mkandarasi mmoja ambaye hakupenda jina lake litaje, alithibitisha kuwa mjengo huo unafikia sh. mil. 400 kwani umechukua nafasi kubwa, na ‘material’ yaliyojengea ni ya gharama.
 
”Ukitazama kwa makini, material nyingi zilizotumika kwenye ujenzi ni zile ya daraja la juu na si hizi za kawaida ambazo watu wengi wamezoea kujengea,” alisema mkandarasi huyo.Jitihada za kumpata Diamond ili aweze kuzungumzia gharama halisi za mjengo huo hazikuzaa matunda kufuatia simu yake ya mkononi kuita bila kupokelewa.

Februari mwaka 2013, nyumba hiyo ikiwa haijakamilika kwa maana ya kupambwa nje na ndani, Diamond alisema imemgharimu sh. mil. 260.Diamond aliripotiwa kuhamia kwenye nyumba hiyo wiki iliyopita, habari za uhakika zinasema kuwa nyota huyo alipata mkosi namba moja baada ya sehemu ya uzio wa upande mmoja kuanguka kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

0 Responses to “THAMANI MJENGO WA DIAMOND BALAA.”

Post a Comment

More to Read