Friday, March 27, 2015
MWENYEKITI WA WAFANYABIASHARA AFUTIWA DHAMANA.
Do you like this story?
Johnson Minja (Kushoto) akiwa mahakamani (Dodoma) |
Mahakama mkoani Dodoma imefuta dhamana ya
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini, Johnson Minja kutokana na
kukiuka masharti ya dhamana aliyopewa ikiwemo ya kutowazuia wafanyabiashara
kufunga maduka yao wakati kesi yake ikiendelea mahakamani
Akitoa taarifa mbele ya hakimu mkazi wa
mahakama ya mkoa wa Dodoma, Rebecca Mbilu, Mwendesha mashtaka wa serikali Rose
Shio amesema kuwa upelelezi dhidi ya kesi hiyo umeshakamilika na kuiomba
mahakama kutengua dhamana ya mshtakiwa kutokana na kukiuka masharti ya dhamana
aliyopewa.
Amesema kuwa pamoja na hilo Mwenyekiti huyo
amekuwa akiendelea kufanya mikutano na wafanyabiashara kwa ajili ya
kuwahamasisha wasiendelee kulipa kodi kwa kutumia mashine za kielektroniki za
efds kitenda alichosema kuwa ni kukiuka masharti ya dhamana aliyopewa.
Hata hivyo wakili wa mshtakiwa, Godfrey
Wasonga ameiambia mahakama kuwa tangu mteja wake apewe dhamana ahajawahi
kuitisha mikutano na wafanyabiashara kwani hata juzi hakuwa na mkutano bali wafanyabiashara
waliokuja mjini Dodoma kusikiliza kesi ya mwenyekiti huyo, waliposikia kuwa
yupo Dodoma walikwenda kumsalimia baada ya kupata taarifa kuwa yuko katika
hoteli ya Image Hill.
Na kuhusu suala la kufunga maduka mwenyekiti
huyo hakuwashawishi wafanyabiashara nchini kufunga maduka yao bali ni
wafanyabishara wenyewe ndo walioamua kufunga maduka yao kwa ajili ya kwenda
kusikiliza kesi ya mwenyekiti wao.
Hata hivyo hakimu Mbilu amesema kuwa
ameridhika na hoja za upande wa mashtaka na hivyo akatengua dhamana ya Minja na
kumtaka kubaki rumande hadi April Mosi mwaka huu ambapo kesi yake itatajwa
tena.
Amesema kuwa kesi hiyo itaanza kusikilizwa
kwa maelezo ya awali April 9 mwaka huu kutokana na ushahidi wa kesi hiyo
kukamilika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MWENYEKITI WA WAFANYABIASHARA AFUTIWA DHAMANA.”
Post a Comment