Wednesday, March 11, 2015

TAARIFA KAMILI YA AJALI YA LEO ENEO LA CHANGALAWE MAFINGA.





Watu 42 wamefariki maeneo ya Changalawe mji mdogo wa Mafinga wilaya ya Mufindi mkoani Iringa baada ya basi la abiria lililokuwa likitokea mkoani Mbeya kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa limetokea Dar es Salaam.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Iringa ACP Ramadhani Mungi amesema tukio hilo limetokea  leo majira ya 09:30 asubuhi ikihusisha basi namba T:438 CDE likitokea mkoani Mbeya kuelekea Dar es Salaam na lori aina ya Scania namba T:689 APK lililokuwa likiendeshwa na dereva Sebastiani Mgama likitokea Dar es Salaam kuelekea Mbeya.


Kamanda Mungi ameongeza kuwa kati ya watu 42 waliofariki kwenye ajali hiyo wanaume ni 33,wanawake 6 na watoto 3 huku maiti nane zimeshatambuliwa na ndugu zao na kuchukuliwa kwa ajili ya shughuli za mazishi.


Aidha amesema maiti hizo zilihifadhiwa  kwa muda katika kituo kidogo cha afya cha Mafinga na kisha kuhamishiwa hospitali ya Rufaa mkoa wa Iringa pamoja na majeruhi 22 wa ajali hiyo ambapo waliojeruhiwa kidogo wataendelea kupata matibabu katika kituo cha afya cha mji mdogo wa Mafinga.


Kamanda Mungi amesema kuwa katika eneo hilo kuna bonde na uchakavu wa barabara,kutokana na mwendo kasi wa dereva wa lori ambaye alikuwa akijaribu kulikwepa shimo lililokuwa katikati ya barabara kabla ya kupishana na basi la abiria.


Amesema kufuatia hali hiyo ikasababisha kupoteza mwelekeo kisha kontena lililokuwa limebebwa na lori hilo kuliangukia basi la abiria ambalo kwa muda huo lilikuwa karibu na lori hilo.


Hata hivo Kamanda Mungi amesema taarifa zaidi zitatolewa kesho Machi 12 ,2015  ambapo pia ametoa wito kwa wamiliki wa magari na madereva kuwa makini wawapo barabarani kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.
MAJINA YALIYOPATIKANA YA ABIRIA WALIOKUWA KATIKA BASI HILO HADI SASA NI: Baraka Ndone  (dereva), Yahya  Hassan ( kondakta), Ester Emanuel, Lusekelo Enock, Jeremia Watson, Digna Solomoni, Frank Chiwango, Luteni Sanga, Teresia Kamingage, Dotto Katuga, Ester Fidelis, Paulina Justine, Mbamba Ipyana, Catherine Mwate, Mwajengo, Ndulile Kasambala, Zera Kasambala, Rebeka Kasambala, Shadrack Msigwa, Mathias Justine, Juliana Bukuku, Cristina Lyimo, Martin Haule na Dominick Mashauri, Omega Mwakasege.   

Wengine ni Ester Willy, Lucy Mtenga, Erick Shitindi, Edwiga Kamiyeye, Frank Mbaula, Mustapher Ramadhani, Kelvin Odubi, Upendo William, Charles Lusenge, Neto Sanga, Pili Vicent, Daniel, Jacob Doketa Iman Mahenge , Juma Sindu, Dk A. Shitindi, Six Erick, Frank Mbaule.

Wengine waliokuwepo katika ajali hiyo wametambuliwa kwa jina moja Amadi, Musa, Elias, Raphael, Hussein na Oswald.


Basi hilo lilianza safari mjini  Mbeya likiwa na abiria 37.

0 Responses to “TAARIFA KAMILI YA AJALI YA LEO ENEO LA CHANGALAWE MAFINGA.”

Post a Comment

More to Read