Saturday, April 4, 2015

CHAMA CHA WANANCHI CUF CHALAANI KAULI YA SPIKA ANNA MAKINDA.




Chama cha Wananchi (CUF) kimelaani kauli ya Spika wa Bunge, Anne Makinda, kwamba anawaburuza wabunge wa upinzani kwa sababu hawafuati utaratibu bungeni.

Makinda alisema hayo alipokuwa akiwajibu wabunge wa upinzani waliolalamika kuburuzwa baada ya Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika, kuomba majibu kutoka kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuhusu kura ya maoni.

Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi a CUF Taifa, Abdul Kambaya, alisema kauli hiyo ya Makinda ni ya dharau, ambayo hazipaswi kutolewa, hasa na kiongozi wa wabunge.

“Spika Makinda anakuwa chanzo cha vurugu bungeni, hasa kwa kuwa mtetezi wa serikali bungeni, badala ya kuwa kiongozi wa Bunge asiyeegemea upande wowote,” Kambaya.

Alisema kitendo cha Spika Makinda kulazimisha kusomwa miswada miwili kuhusu habari na matumizi ya mitandao ya kijamii, hakikubaliki kwa Watanzania na kinadhihirisha kishachoka kuliongoza Bunge.


CUF tunamuonya Spika Makinda aache ukada wa CCM na kuiegemea serikali wakati maslahi ya wananchi yanavunjwa na kukanyagwa,” Kambaya.

Alimtaka Spika Makinda kutambua kuwa iwapo ataendelea na utaratibu huo, atalivuruga Bunge na kutowesha amani.

0 Responses to “ CHAMA CHA WANANCHI CUF CHALAANI KAULI YA SPIKA ANNA MAKINDA. ”

Post a Comment

More to Read