Saturday, April 4, 2015

CHARLES HILARY AONDOKA BBC SWAHILI, SASA KUJIUNGA NA AZAM TV




Miongoni mwa watu ambao sauti zao zimesikika sana kupitia BBC London, ni Mtangazaji Mtanzania Charles Hillary aliyewahi kusikika sana hata kupitia Radio One pia.

Charles Hillary sasa anarudi nyumbani Tanzania na kujiunga na kituo cha Televisheni cha Azam ambapo mhariri wa BBC Afrika Dar es salaam Solomon Mugera aliwaambia wafanyakazi wake kuhusu kuondoka kwa Hillary.

Naibu Mtendaji mkuu wa Azam Tido Muhando alithibitisha Hillary kutarajiwa kujiunga na Azam Media akiwa na historia nzuri kwenye vyombo vya habari kuanzia alipoanza mwaka 1994 Radio one na kabla ya hapo alitokea radio Deutsch Welle na mwaka 2006 alijiunga na BBC.


0 Responses to “ CHARLES HILARY AONDOKA BBC SWAHILI, SASA KUJIUNGA NA AZAM TV ”

Post a Comment

More to Read