Saturday, April 4, 2015
MOROCCO YASHINDA KESI CAS, SASA YATAMBA KUWA MWENYEJI AFCON.
Do you like this story?
KIONGOZI wa juu wa Shirikisho la soka nchini Morocco, Nour Eldin
Boushehati ameweka wazi kuwa taifa lake liko tayari kuwa mwenyeji wa fainali za
mataifa ya Africa, Afcon 2017.
Mahakama ya juu ya rufani ya FIFA ya masuala ya mpira (CAS)
alhamisi ya wiki hii iliitangaza Morocco kuwa huru kutoka katika kifungo
cha CAF na kusema wanaweza kushiriki fainali za Afcon 2017 na 2019.
Boushehati sasa anajiamni kuwa wako tayari kuhodhi michuano hiyo
kwa miaka miwili mfululizo.
"Tuko yatari kuwa wenyeji wa michuano ijayo ya Afcon
kama serikali itatupa ruksa, tuko tayari, tunaisikiliza serikali.
Wakituruhusu tutakuwa tayari kuwa wenyeji," Amesema Boushehati.
Morocco walitakiwa kuwa wenyeji wa fainali za Afcon mwaka huu
2015 lakini walichomoa dakika za mwisho wakihofia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.
Guinea ya Ikweta ilikubali kuwa mwenyeji wa fainali hizo muda
mfupi baada ya kuombwa na CAF.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MOROCCO YASHINDA KESI CAS, SASA YATAMBA KUWA MWENYEJI AFCON.”
Post a Comment