Wednesday, April 1, 2015

KAULI YA MWAMBUSI KUIKABILI NDANDA FC HII HAPA....




KOCHA mkuu wa City Juma Mwambusi amesema anafahamu  kuwa kikosi chake kitacheza  mchezo ujao wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya Ndanda Fc  ugenini kwenye  uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoni Mtwara lakini amejiandaa vizuri kupambana kutafuta matokeo.

 Mwambusi amesema kuwa  ligi ya msimu huu ni ngumu, tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita ambapo timu nyingi zilijiandaa vizuri toka mwanzo wa msimu huku changamoto ya kutafuta nafasi kwenye msimamo wa ligi ikichagiza  kuwepo kwa ushindani mkubwa.

“Kila mmoja anafahamu  msimu ligi ni ngumu, lakini kama mwanasoka siku zote unatakiwa kuwa sawa kwa maana ya utayari wa kupambana wakati wowote, tunakwenda kucheza ugenini, nia yetu wote ni kushinda ingawa kwenye soka kuna matokeo matatu, tunakwenda kupambana kwa ajili ya kutafuta matokeo, imani yangu kwa uwezo wa mwenyezi mungu City itapata ushindi” alisema Mwambusi.

“City iliyo kwenye nafasi ya tisa hivi sasa kwenye msimamo wa ligi itashuka uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoni Mtwara, jumamosi ya tarehe 4 katika mwendelezo wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara dhidi ya wenyeji Ndanda Fc walio katika nafasi ya 11.

0 Responses to “KAULI YA MWAMBUSI KUIKABILI NDANDA FC HII HAPA....”

Post a Comment

More to Read