Wednesday, April 1, 2015
RAIS WA NIGERIA NI MUHHAMADU BUHARI.
Do you like this story?
Mwenyekiti wa Tume ya
Uchaguzi nchini Nigeria,INEC, Attahiru Jega amemtangaza rasmi Kiongozi wa wa
chama cha upinzani cha Nigeria jenerali Muhammadu Buhari kuwa rais wa taifa
hilo kubwa barani Afrika baada ya kumbwaga rais wa zamani Goodluck Jonathan.
Tayari rais anayeondoka madarakani Goodluck
Jonathan amekwisha kubali kushindwa kwake baada ya kumpigia simu mpinzani wake,
Jenerali Buhari na kumpongeza kwa ushindi huo wa kihistoria.
Hii inakuwa mara ya kwanza katika historia ya
taifa hilo kwa rais wa nchi hiyo kung'olewa madarakani na kiongozi wa upinzani.
Wadadisi wa maswala ya ndani wanasema kuwa
inaonekana kuwa Nigeria sasa imekomaa kisiasa haswa baada ya kushuhudia
mapinduzi kadha ya kijeshi tangu ipate uhuru wake kutoka kwa Uingereza mwaka wa
1960.
Hata hivyo kumekuwa na taharuki kubwa haswa
baada ya tume ya uchaguzi kuchelewa kutoa matokeo ya uchaguzi.
Hofu ingalipo kuwa huenda wafuasi wa wagombea
hao ambao wanatofautia kimsingi katika maswala kadha ikiwemo ya kidini na vile
vile kimajimbo .
Wanigeria wengi wamefurahi kuwa hatimaye
wameweza kuing'oa mamlakani serikali ambayo haikuwa ikitekeleza majukumu yake
kikamilifu.
Buhari angali hajatangazwa rasmi kuwa mshindi
na tume hiyo japo alikuwa amefungua pengo la zaidi ya kura milioni tatu dhidi
ya mpinzani wake wa karibu rais Goodluck.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “RAIS WA NIGERIA NI MUHHAMADU BUHARI.”
Post a Comment