Wednesday, April 1, 2015

MSANII SUMA LEE APIGA MARUFUKU NYIMBO ZAKE KUPIGWA RADIONI ,ASEMA SASA YEYE MUZIKI WA KIDUNIA BASI.






Hit maker wa ‘Hakunaga’, Suma Lee amesema kuwa hatafanya tena muziki
kwasababu ameachana kabisa na maisha hayo na ameamua kusomea dini ya
kiislam
Suma ambaye alitengeneza pesa nyingi kupitia hit yake ya ‘Hakunaga’,
amesema kuwa hana mpango wa kuzitoa nyimbo zake zilizoko studio ambazo
hazijatoka.

“sifanyi tena muziki na nimeachana kabisa na maisha hayo, na nyimbo zote
zilizobaki studio nimezisimamisha zisitoke baada ya kuzilipia, “
Alisema Suma.

“kuna wimbo mmoja nimefanya na Cp ambao ndio ulikuwa wa kurudisha kundi
la Parklane, pia nimeuzuia, labda Cp auchukue yeye.Kilichobaki ni
kuwaombea wazazi wetu waliotutangulia, wengine walikuwa hawataki tufanye
kazi hizi, kwa kuwa hawapo na hakuna wakutukataza tena, bora tukae na
kuwaombea.”

0 Responses to “MSANII SUMA LEE APIGA MARUFUKU NYIMBO ZAKE KUPIGWA RADIONI ,ASEMA SASA YEYE MUZIKI WA KIDUNIA BASI.”

Post a Comment

More to Read