Saturday, April 18, 2015

NEC: UCHAGUZI MKUU HAUTASOGEZWA MBELE.


Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Manunuzi na Logistic, Gregory Kaijage na kushoto ni Naibu Katibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mkuu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), Sisti Chriati.

Baadhi ya Wandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano wa habari wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi jijini Dar es Salaam jana.


TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuwa, Uchaguzi Mkuu utafanyika kama ulivyopangwa na haiwezi kusegeza mbele tarehe ya uchaguzi huo kutokana na suala hilo kuwa ni la kikatiba.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa wanasiasa wamekuwa na kauli ambazo zinawafanya wananchi wapate hofu wakati suala hilo kuhairisha uchaguzi halipo katika tume.

jaji Lubuva ameongeza kuwa wanasiasa wanatakiwa kuangalia maneno ambayo wanayatoa kwani hayana msingi, wanatakiwa watoe sera zao za vyama kwa wananchi na sio kuisemea tume mambo ambayo hayana ukweli wowote.

Amesema pia kuwa, zoezi la kuandikisha kwa Mkoa wa Njombe ambalo linaisha leo na kuhamia katika mikoa ya Iringa, Lindi, Ruvuma pamoja na Mtwara ambalo litaanza Aprili 24 mwaka huu.

Lubuva amesema wanatarajia kupokea vifaa vya kuandikisha kwa kuchukua alama za vidole (BVR)1600 ambazo zitafanya kazi katika mikoa hiyo na kuhamia Mikoa ya Dodoma, Mbeya, Katavi pamoja na Rukwa kuongezeka BVR tena 1600 na BVR 1,152 zitafanya kazi katika mikoa Singida, Tabora, Kigoma pamoja na Kagera na uandikishaji utaanza Mei 2 mwaka huu.

Aidha amesema zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la mpiga kura litamalizika Julai mwaka  huu hivyo wananchi wajiandae katika kupiga kura  katika uchaguzi mkuu wa Oktoba.

Jaji Lubuva amesema Rais Jakaya Kikwete anataka amalize ili apumzike hivyo hakuna mpango wowete wa kuongeza muda wa uongozi kwake.
 (Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii)

0 Responses to “NEC: UCHAGUZI MKUU HAUTASOGEZWA MBELE.”

Post a Comment

More to Read