Wednesday, April 15, 2015

TWIGA STARS YAPEWA TENA ZAMBIA KUFUZU U-20 KOMBE LA DUNIA.




Na Bertha Lumala, Dar es Salaam 
'Twiga Stars imeing'oa Shepolopolo kwa jumla ya mabao 6-5 katika kuwania kufuzu michuano ya Olimpiki ijayo.'

TIMU ya taifa ya wanawake ya Tanzania (Twiga Stars) ya U-20 imepangwa kuchuana dhidi ya timu ya taifa ya wanawake ya Zambia (Shepolopolo) katika kuwania kufuzu fainali zijazo za Kombe la Dunia kwa vijana wenye umri huo zitakazofanyika mwakani nchini Guinea.

Hivi karibuni Twiga Stars iliing'oa Shepolopolo kwa jumla ya mabao 6-5 katika kuwania kushiriki michuano ya Olimpiki ijayo.

Katika droo iliyochezeshwa mchana huu na Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), Tanzania imepangwa kuchuana na Zambia tena, Twiga Stars ikianzia nyumbani kati ya Julai 10-12 mwaka huu kabla ya kurudiana Lusaka, Zambia Julai 24-26 mwaka huu.

Nchi nyingine zitachuana kama ifuatavyo:

Djibouti vs Burkina Faso
DR Congo vs Gabom
Sierra Leone vs Liberia


Algeria itachuana na mshindi kati ya Djibouti vs Burkina Faso wakati Cameroon itachuana na Ethiopia.

Guinea ya Ikweta vs Mali
Ghana vs Senegal

Mshindi kati ya DR Congo vs Gabon atachuana na Namibia wakati mshindi kati ya Sierra Leone na Liberia atachuana dhidi ya Nigeria.

0 Responses to “TWIGA STARS YAPEWA TENA ZAMBIA KUFUZU U-20 KOMBE LA DUNIA.”

Post a Comment

More to Read