Wednesday, April 15, 2015

MAYWEATHER KUSTAAFU MASUMBWI.


Siku zinazidi kukatika kuelekea pambano lenye thamani kubwa zaidi kuwahi kutokea duniani, wengine wanaliita pambano la karne baina ya bondia asiyepigika Flody Mayweather  na Manny Pacquiao litakalopigwa mei pili mwaka huu Las Vegas Marekani.
 
Habari mpya kutoka kwa Mayweather ni kwamba baada ya pambano la mwezi mei amekiri kuwa ataongeza pambano lingine moja mwezi septemba na baada ya hapo atastaafu mchezo wa masumbwi.

Bondia huyo tajiri amesema sasa hafurahii tena mchezo huo na inamlazimu kukaa pembeni ili kufanya mambo mengine.

0 Responses to “MAYWEATHER KUSTAAFU MASUMBWI.”

Post a Comment

More to Read