Friday, May 15, 2015

JUMA MWAMBUSI ATAJA KIKOSI BORA CHA LIGI KUU TANZANIA BARA 2014/2015


Juma Mwambusi, kocha mkuu wa Mbeya City fc


TUNAENDELEA na zoezi letu la kuangalia vikosi bora vya makocha wa timu za ligi kuu soka Tanzania bara, makocha wasiokuwa na timu na wachambuzi wa soka kwa msimu wa ligi kuu wa 2014/2015 uliomalizika mei 9 mwaka huu,  Yanga wakiibuka mabingwa, Azam nafasi ya pili, Simba nafasi ya tatu na Mbeya City nafasi ya nne.
 
Siku mbili zilizopita tumeweza kukuletea kikosi bora cha kocha wa Yanga , Hans van der Pluijm na Coastal Union, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, lakini leo tunakuletea kikosi bora cha msimu kilichopendekezwa na kocha bora wa msimu wa 2013/2014, Juma Mwambusi.
 
Kwanza Mwambusi amesema: “Ligi ilikuwa ngumu, kama unavyojua mwaka jana tuliingia na changamoto mpya na msimu uliomalizika (2014/2015) timu zilijidhatiti sana. Lakini kama mwalimu pamoja na kucheza mechi ngumu, mtazamo wangu ulikuwa kuangalia wachezaji ambao ninaweza kuwapendekeza katika kikosi ambacho kinaweza kucheza timu yoyote na  kuleta mafanikio”.
 
HIKI NDICHO KIKOSI BORA CHA VPL 2014/2015 KILICHOPENDEKEZWA NA JUMA MWAMBUSI

  1.Hanington Kalisebula (Mbeya City)
2.Hassan Ramadhan Kessy (Simba)
3. Hassan Mwasapili (Mbeya City)
4.Serge Paschal Wawa (Azam fc)
5. Salim Mbonde (Mtibwa Sugar)
6. Steven Mazanda (Mbeya City)
7.  Simon Msuva (Yanga)
8. Haruna Niyonzima (Yanga)
9. Paul Nonga (Mbeya City)
10.  Amissi Tambwe (Yanga)
11.  Emmanuel Okwi (Simba)

0 Responses to “JUMA MWAMBUSI ATAJA KIKOSI BORA CHA LIGI KUU TANZANIA BARA 2014/2015”

Post a Comment

More to Read