Thursday, May 7, 2015
MWIGIZAJI SALMAN KHAN WA BOLLYWOOD KWENDA JELA MIAKA 5 KWA KOSA LA KUUWA!!
Do you like this story?
Mwigizaji maarufu wa filamu za Bollywood nchini India Salman Khan
amekuhumiwa kifungo cha miaka mitano jela baada ya kupatikana na hatia ya
kumuua mtu mmoja asiye na makazi alipokuwa akiendesha gari huku akiwa amelewa
mjini Mumbai.
Khan alikuwa ameshtakiwa kwa kuua
bila kukusudia baada ya kuelekeza gari lake kwenye kundi la watu waliokuwa
wamelala kwenye njia kando ya barabara mwaka 2002. Mmoja kati ya watu hao Noor
Ullah Khan alikufa katika ajali hiyo.
Khan amedai kuwa dereva wake ndiye
anayepaswa kulaumiwa lakini mashuhuda wanasema mwigizaji huo ndiye aliyekuwa
kwenye usukani na alikimbia baada ya kutokea kwa ajali hiyo.
Kwa mujibu wa jaji wa mahakama
hiyo mwigizaji huyo anaweza kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MWIGIZAJI SALMAN KHAN WA BOLLYWOOD KWENDA JELA MIAKA 5 KWA KOSA LA KUUWA!!”
Post a Comment