Wednesday, May 13, 2015
RAIS NKURUNZINZA APINDULIWA.
Do you like this story?
Ripoti kutoka Bujumbura zinasema kuwa kamanda
mmoja wa kijeshi ametangaza kuwa hamtambui tena Pierre Nkurunziza kama rais wa
Burundi
Meja Jenerali Godefroid Niyombareh amewaambia
waandishi wa habari mjini Bujumubura, kuwa kumeundwa kamati maalum ya kuiokoa
Burundi itakayotawala taifa hilo kwa kipindi cha mpwito.
Kulingana na taarifa iliyopeperushwa na redio
Isanganiro, serikali ya Nkurunziza imeon'golewa madarakani.
Meja Generali Niyombareh amesema wamechukua
hatua hiyo baada ya watu wa Burundi kukataa kwa kinywa kipana awamu ya tatu ya
urais wa Nkurunziza.
Jenerali huyo aliyetimuliwa na Nkurunziza
mwezi februari anasema kuwa Nkurunziza alishindwa kuheshimu mwafaka wa amani
mbali na sheria za kimataifa.
Kwa sasa rais Nkurunziza yuko nchini Tanzania
alipokuwa anatarajiwa kujumuika na viongozi wa kanda hii ya Afrika Mashriki
kutafuta suluhu ya mgogoro wa Burundi tangu Nkurunzinza atangaze nia yake ya
kuwania awamu ya tatu.
Jenerali Niyombareh alikuwa ameandamana na
viongozi wengine wa jeshi la Burundi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “RAIS NKURUNZINZA APINDULIWA.”
Post a Comment