Thursday, July 9, 2015

BOBBY BROWN AOMBA MSAMAHA KWA KUSAHAU MASHAIRI





GEORGIA, Marekani
MWANAMUZIKI wa kimataifa wa R&B, Bobby Brown hivi karibuni aliwaomba msamaha mashabiki waliohudhuria kwenye tamasha lake huko Atlanta, Georgia baada ya kusahau mashairi ya wimbo aliokuwa anaimba hali iliyosababisha yeye na madensa wake kupishana jukwaani.

Bobby hakuonekana kabisa mwenye furaha katika tamasha hilo ambalo ni la pili kufanya tangu Januari alipoanza kumuuguza bintiye, Bobbi Kristina kitendo kilichosababisha watu wengi kujiongeza kuwa huenda hali mbaya zaidi aliyonayo bintiye kwa sasa inamvuruga.

“Samahani, siko katika hali ya kawaida usiku huu ingawa nafahamu wote mnanisikia vizuri na kucheza nami.Lakini bado ni fahari kuwa hapa,” msanii huyo aliwaambia wahudhuriaji baada ya kusimamisha muziki katikati ya tamasha kufuatia tukio hilo.

0 Responses to “BOBBY BROWN AOMBA MSAMAHA KWA KUSAHAU MASHAIRI”

Post a Comment

More to Read