Sunday, July 12, 2015
IJUE HISTORIA YA MAGUFULI KWA UFUPI KABLA YA KUTEULIWA.
Do you like this story?
Dk. John Pombe Joseph Magufuli, alizaliwa Oktoba 29, 1959
wilayani Chato – wakati huo ikiwa Mkoa wa Kagera (sasa Mkoa wa Geita).
Ana Shahada ya Uzamivu ya Kemia (2006 – 2009) kutoka Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam.
Mwaka 1991 – 1994, alisoma Shahada ya Uzamili (Kemia) katika
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na baadaye Chuo Kikuu cha Salfordnchini
Uingereza.
Mwaka 1985 – 1988, alisoma Shahada ya Kwanzaya Elimu katika
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akichukua masomo ya Kemia na Hisabati.
Mwaka 1981 – 1982, alisoma diploma katika Chuo cha Mkwawa
akichukua masomo ya Kemia na Hisabati.
Mwaka 1979 – 1981, alipata elimu ya juu ya sekondari katika
Shule ya Sekondari Mkwawa, Iringa.
Mwaka 1977 – 1978, alisoma elimu ya sekondari katika Shule
ya Sekondari Lake, Mwanza.
Mwaka 1975 – 1977, alisoma Shule ya Msingi Katoke,
Biharamulo mkoani Kagera.
Mwaka 1967 – 1974, alisoma Shule ya Msingi, Chato.
Mafunzo
Machi 1984 – Juni 1984 alihudhuria mafunzo ya Jeshi la
Kujenga Taifa (JKT), Mpwapwa mkoani Dodoma.
Januari 1984 – Machi 1984 alikuwa JKT Makuyuni, Arusha.
Julai 1983 – Desemba 1983 alikuwa JKT Makutupora, Dodoma.
Uzoefu wa kazi
Mwaka 2010 – hadi sasa: Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Chato.
Mwaka 2008 – 2010: Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Samaki;
Mbunge wa Biharamulo Mashariki (Chato).
Mwaka 2005 – 2008: Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi; na Mbunge wa Biharamulo Mashariki (Chato)
Mwaka 2000 – 2005: Waziri wa Ujenzi, na Mbunge wa Biharamulo
Mashariki.
Mwaka 1995 – 2000: Naibu Waziri wa Ujenzi; na Mbunge wa
Biharamulo Mashariki.
Mwaka 1989 – 1995: Mkemia Chama cha Ushirika cha Nyanza
Cooperative Union (Ltd.),Mwanza.
Mwaka 1982 – 1983: Mwalimu Shule ya Sekondari Sengerema
(akifundisha masomo ya Kemia na Hisabati).
Dk. Magufuli amepata tuzo mbalimbali za ndani na nje ya
nchi.
Ameshiriki na kuongoza mikutano mingi ya kitaifa na
kimataifa.
Ameandika vitabu na majarida mbalimbali. Ameoa na ana watoto
kadhaa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “IJUE HISTORIA YA MAGUFULI KWA UFUPI KABLA YA KUTEULIWA.”
Post a Comment