Friday, July 3, 2015

MSERBIA WA SIMBA APIGA MARUFUKU VYAKULA HIVI....




KOCHA wa viungo wa Simba, Mserbia Dusan Mumcilovis, ameshangazwa na kitendo cha wachezaji wa timu hiyo kulishwa wali mweupe kwa maharage, akitaka wapewe vile vinavyofaa kutumiwa na wanamichezo kama ilivyo kwa nyota wa Ulaya, wakiwamo Cristiano Ronaldo wa Real Madrid. 

Akifanya mahojiano na BINGWA jana wakati wa mazoezi ya timu hiyo kwenye Uwanja wa TCC Chang’ombe, Dar es Salaam, Mumcilovis alisema kuwa si vyema kwa wachezaji wake kulishwa vyakula laini, ikiwamo soda zenye kemikali kama Pepsi, CocaCola na Sprite, badala yake walitakiwa kula vile vyenye virutubisho zaidi ya viwili kama pilau lenye viungo vingi, maji mengi, matunda, juisi za matunda (fresh), maziwa na vinginevyo vya kuujenga mwili.

Alisema kwa klabu kama Simba, wachezaji wake wanastahili kula vyakula kama wanavyokula wachezaji wa Ulaya na kwa utaratibu maalumu si bora kujaza matumbo.

0 Responses to “MSERBIA WA SIMBA APIGA MARUFUKU VYAKULA HIVI.... ”

Post a Comment

More to Read