Friday, July 3, 2015
BOKO HARAM YASHAMBULIA ZAIDI
Do you like this story?
Watu 150 wameuawa
baada ya Boko Haram kuvamia kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Walioshuhudia mashambulizi hayo wanasema watu
tisini na saba wameuawa siku ya Jumatano katika kijiji cha Kukawa kilichopo
karibu na Ziwa Chad.
Habari zinasema pia wanaume 48 wamepigwa
risasi na wapiganaji katika mashambulizi tofauti siku ya Jumanne.
Mashuhuda wanaokimbia eneo lililopo karibu na
Ziwa Chad wanasema idadi kubwa ya wapiganaji wamevamia vijiji vitatu ambapo
wameuwa wanaume, wanawake na watoto.
Baadhi ya ripoti zinasema walipigwa risasi
huku wengine wakielezea jinsi wapiganaji hao walivyowachinja watu na kuchoma
majengo.
Upande wa Kusini, nje kidogo na mji wa
Monguno, kundi la wapiganaji wa Boko Haram wamefika usiku wakati watu
walipokuwa wanaswali. Waliwasubiri mpaka walipomaliza kuswali na kuwatenganisha
wanaume na wanawake na baadae kuanza kuwamiminia risasi wanaume.
Mwanasiasa anayewakilisha eneo hilo, Mohammed
Tahir amesema awali alitoa tahadhari kwa jeshi la Nigeria kwamba vijiji hivyo
viko hatarini kwa sababu Boko Haram wameweka makazi katika maeneo hayo baada ya
kutimuliwa katika himaya yao ya msitu wa Sambisa.
Haya ni mashambulizi mabaya zaidi kufanywa na
Boko Haram katika kipindi cha wiki kadhaa.
Kundi hilo limekuwa likilipuwa mabomu kadhaa
baada ya kudhoofishwa na majeshi ya Nigeria.
Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari amesema
kipaumbele chake ni kuimarisha mapambano dhidi ya Boko Haram.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ BOKO HARAM YASHAMBULIA ZAIDI”
Post a Comment