Monday, September 28, 2015
CELINA KOMBANI KUAGWA LEO DAR
Do you like this story?
Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mbunge wa Ulanga Mashariki (CCM), Bi. Celina Kombani. |
Mwili wa Marehemu Kombani ulivyoshushwa Uwanja wa Ndege wa Mwl. Nyerere kutoka India, juzi. |
Mwili
wa aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Mbunge wa Ulanga Mashariki (CCM), Bi.
Celina Kombani utaagwa rasmi leo
Jumatatu, kuanzia majira ya saa nne asubuhi katika Viwanja vya Karimjee jijini
Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Bunge, baada ya zoezi la kuaga mwili
wa marehemu na kutoa heshima za mwisho, utasafirishwa kwenda mkoani Morogoro
kuanzia majira ya saa tisa alasiri ambapo utalala nyumbani kwake Forest Hill.
Jumanne
kuanzia majira ya saa nne asubuhi, itafanyika ibada maalum ya mazishi na
baadaye mwili utaagwa katika Viwanja vya Jamhuri mjini Morogoro na kufuatiwa na
mazishi shambani kwake, Lukobe nje kidogo ya mji wa Morogoro.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “CELINA KOMBANI KUAGWA LEO DAR”
Post a Comment