Monday, September 14, 2015
MKICHAGUA UKAWA NAWAHAKIKISHIA MTAPATA KITUO CHA AFYA.
Do you like this story?
Mgombea mwenza
wa urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia chama cha demokrasia na
maendeleo (CHADEMA ),anayewakilisha vyama vinavyounda umoja wa katiba ya
wananchi ( UKAWA) Mh. Juma Duni Haji ameendelea na mikutano ya kampeni za
kumnadi mgombea urais wa chama hicho Mh. Edward Lowassa katika mkoa wa rukwa na
kuhaidi kuwa UKAWA ikiingia madarakani,serikali itawajengea wananchi wa jimbo
la kwela kituo cha afya, barabara na kuwapatia huduma ya majisafi na salama kwa
kutumia mapato ya sekta ya madini peke yake
Akiwahutubia wananchi
wa vijiji vya ilemba,mto wisa na muze vilivyoko katika bonde la ziwa
rukwa,jimbo la kwela sumbawanga vijijini katika mikutano ya hadhara ya kampeni
za uchaguzi mkuu – mgombea mwenza huyo wa urais wa chadema chini ya mwavuli wa
vyama vinne vinavyounda ukawa,Mh. Juma Duni Haji amesema ni jambo la
kusikitisha kuona wakazi wa bonde hilo la ufa wakiishi maisha ya dhiki na
kuwaomba watanzania kumchagua Mh.Edward Lowassa Oktoba 25 mwaka huu ili aweze
kubadili hali zao za maisha kwa kuwaletea maendeleo.
Aliyewahi kuwa mbunge
wa jimbo la mkanyageni Pemba kupitia chama cha wananchi( CUF ),Mohammed Habib
Mnyaa pamoja na mwenyekiti wa chadema mkoa wa Rukwa Zeno Lukoswe wamesema laiti
kama serikali ya chama cha mapinduzi ingewekeza katika bonde hilo,lingechangia
kukuza utalii na kuongeza mapato ya serikali badala ya kulitelekeza na
kusababisha umaskini kwa wakazi wanaoishi ndani ya bonde hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MKICHAGUA UKAWA NAWAHAKIKISHIA MTAPATA KITUO CHA AFYA.”
Post a Comment