Friday, September 18, 2015

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI KUHUSU TATHIMINI YA UCHAGUZI 2015




Akiongea na waandishi wa habari, msemaji wa jeshi la polisi, Advera Bulimba..’Katika kipindi hiki knachoendelea cha kampeni hali ya usalama inaonekana ni shwari hakuna matukio makubwa ambayo yaliyoripotiwa yakushtua tunawashukuru wananchi lakini pia viongozi wa vyama vya siasa na wafuasi wao ambao wamekuwa wakitii sheria za nchi’ – Advera Bulimb
 
‘Hata hivyo pamoja na ushwari huo bado kumejitokeza baadhi ya watu wachache kufanya vitendo vya uhalifu vyenye mweleko wa kuvunja amani ambayo hata hivyo wameweza kuthibitiwa na jeshi la polisi jumla ya matukio 107 yameripotiwa katika vituo vya polisi kati ya matukio hayo matukio 38 tayari yamefunguliwa kesi na kufikishwa mahakamani’ – Advera Bulimba

‘Hayo matukio 38 ambayo yafunguliwa kesi na kufikishwa mahakamani yana jumla ya watuhumiwa 52 ambao tayari tumewafikisha mahakamani ili sheria iweze kuchukua mkondo wake, aidha matukio mengine yaliyobaki 68 bado yapo chini ya upelelezi wa jeshi la polisi, katika matukio hayo ambayo tumeyafikisha mahakamani wengi wanatuhumiwa kuvunja kufanya makosa yafuatayo ikiwemo wafuasi wa chama kimoja kuvamia ama kuzomea wafuasi wa chama kingine hususani wanapokuwa katika kampeni za uchaguzi maeneo mbalimbali ya mikoani‘ – Advera Bulimba


0 Responses to “TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI KUHUSU TATHIMINI YA UCHAGUZI 2015”

Post a Comment

More to Read