Sunday, September 20, 2015
WANAFUNZI WATAKIWA KUONGEZA BIDII KATIKA MASOMO YA SAYANSI.
Do you like this story?
Na.
Jovina Bujulu –MAELEZO.
Wanafunzi
wanaosoma masomo ya Sayansi kote nchini wameshauriwa kuongeza bidii katika
kujifunza masomo hayo ili kuendana na juhudi zinazofanywa na Serikali za
kuwawezesha wanafunzi hao kujifunza masomo ya Sayansi kwa vitendo.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mkemia Mkuu wa Serikali Prof. Samweli
Manyele kwenye sherehe ya kuwapongeza wanafunzi 24 wa kidato cha nne na sita
waliofanya vizuri katika masomo ya Kemia na Biolojia kwa mwaka 2013 na 2014.
“Kama
wachunguzi wa Serikali ambao hutumia taaluma zitokanazo na masomo ya Kemia na
Biolojia tumeona ni Vizuri kutoa hamasa kwa vijana na Taifa hili kupenda masomo
ya Sanyansi” Amesema Prof. Manyele.
Amesema
Zoezi la kuwapongeza na kuwazawadia wanafunzi wanaofanya vizuri kwenye masomo
ya Kemia na Biolojia limeanzishwa kutoakana na Wakala ya Mkemia Mkuu wa
Serikali kupewa jukumu la kusimamia Sheria ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali
za Viwandani na Majumbani.
Aidha,
amesema Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kitagharamia masomo ya Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano kwa walimu na wanafunzi wanne ili waweze kuimarisha
vipaji vyao vya masomo na matumizi ya kompyuta .
Amefafanua
kuwa Katika sherehe hizo jumla ya wanafunzi 24 na walimu 4 kutoka shule
mbalimbali za Sekondari hapa nchini wamezawadiwa vitu mbalimbali zikiwemo
Fedha, Vyeti na Santuri kwa ajili ya kujifunza zaidi masomo ya Sayansi kwa
upande wa wanafunzi na walimu kujifunza mbinu zaidi za kufundisha masomo hayo.
Kwa
upande wa Wanafunzi waliozawadiwa amesema wanatoka shule za Sekondari za Feza,
Marian, Iliboru, St. Francis na Shule ya Sekondari ya Kata ya Nyamanoro iliyoko
jijini Mwanza.
Sherehe za kuwazawadia na kuwapa
tuzo mbalimbali wanafunzi wa masomo ya Sayansi zilianzishwa mwaka 2007 chini ya
Mkemia Mkuu wa Serikali, huambatana na utoaji wa zawadi na tuzo mbalimbali kwa
wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo ya Kemia na Bioloji
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WANAFUNZI WATAKIWA KUONGEZA BIDII KATIKA MASOMO YA SAYANSI.”
Post a Comment