Thursday, October 8, 2015
-KIWANDA BUBU CHA KUSINDIKA SEHEMU ZA SIRI ZA N"GOMBE CHAFUNGWA
Do you like this story?
Hatimaye,
Halmashauri ya manispaa ya Ilala imekifunga rasmi kiwanda bubu
kinachosindika sehemu nyeti za Ng'ombe Dume, kutokana na kufanya kazi zao
katika makazi ya watu,huku kukiwa na mazingira machafu na kusababisha harufu
kali katika eneo la Tabata bima mtaa wa umoja jijini Dsm.
Kufungwa kwa kiwanda hicho Bubu ambacho pia kimekuwa
kikikusanya pembe za ng'ombe na kusafirisha nchini China, kumetokana na
malalamiko kutoka wananchi ambao walikuwa wakilalamikia harufu kali, inzi na
mazingira machafu ya eneo hilo.
Aidha wamiliki hao raia wa kichina pamoja na kufungiwa rasmi
wamepigwa faini ya shilingi millioni kumi, kutokana na kuendesha shughuli zao
katika mazingira machafu hali inayoweza kueneza magonjwa.
Mmoja wa wafanyakazi katika eneo hilo amesema nyeti hizo za
ng'ombe zimekuwa zikiletwa na kukaushwa eneo hilo na baadae kusafirishwa kwenda
china kwa ajili ya kutengeneza dawa za kuongeza nguvu za kiume maarufu Viagra.
Katika eneo hilo pia kimebainika kiwanda cha kutengeneza vitu
mbali mbali vya ndani ikiwemo sahani za plastic huku zikiwa zimebandikwa lebo
kutoka china ambapo baada ya kutakiwa kuonyesha vibali walishindwa
kuonyesha na kudai kiwanda hicho kipo katika hatua za majaribio.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “-KIWANDA BUBU CHA KUSINDIKA SEHEMU ZA SIRI ZA N"GOMBE CHAFUNGWA”
Post a Comment