Thursday, October 8, 2015

MCHUNGAJI PETER MSIGWA APANDISHWA MAHAKAMANI KWA KUWAJERUHI POLISI




MGOMBEA Ubunge jimbo la Iringa Mjini kupitia Chadema, Mchungaji Peter Msigwa na wenzake watatu, wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Mkoa wa Iringa wakituhumiwa kushambulia na kujeruhi askari polisi wawili.

Katika mashitaka hayo, Msigwa ambaye alikuwa Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini na Waziri kivuli katika Wizara ya Maliasili na Utalii katika bunge lililopita, alifikishwa na wenzake watatu shitaka linalowakabili washitakiwa 10 kwa makosa hayo.

 Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Blandina Manyanda aliwataja washitakiwa wengine waliofikishwa mahakamani hapo mbele ya Hakimu Makazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Iringa, David Ngunyale, kuwa ni Edwine Sambala(66), Joseph Mgima (56) na Josephat Chengula (36).

Manyanda alisema kuwa washitakiwa hao walitenda makosa hayo Septemba 28 mwaka huu, ambapo watuhumiwa hao kwa pamoja walifanya makosa hayo kwa kufanya kosa la uvunjifu wa amani katika eneo Sambala Kata ya Gangilonga na kuwasababishia usumbufu kwa watumiaji wa barabara ya Iringa Dodoma.

 

0 Responses to “ MCHUNGAJI PETER MSIGWA APANDISHWA MAHAKAMANI KWA KUWAJERUHI POLISI”

Post a Comment

More to Read