Thursday, November 12, 2015

.CHAMA CHA ACT WAZALENDO KIMEMTAKA RAIS DK MAGUFULI KUINGILIA KATI SAKATA LILILOPO ZANZIBAR




Chama cha ACT Wazalendo kimemtaka rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli kuingilia kati sakata lililopo visiwani Zanzibar kwa sababau Tanzania haijakamilika kama Zanzibar haipo. 

Akizungumza jijini Dar es Salaam kiongozi mkuu wa chama hicho Mh Zitto Kabwe amesema kitendo cha kutokuchukuliwa kwa hatua kwa mambo yanayoendelea Zanzibar siyo sawa na hivyo rais Magufuli amshinikize mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar kutangaza matokeo.

Naye mwenyekiti wa chama hicho Bi Anna Mgwira amabaye alikuwa ni miongoni mwa wegombea urais amesema wanashukuru uchaguzi umeisha na wataendeleza mipango yao kama kawaida na wanashukuru kuwa serikali ya awamu ya tano imeanza vyema.

0 Responses to “.CHAMA CHA ACT WAZALENDO KIMEMTAKA RAIS DK MAGUFULI KUINGILIA KATI SAKATA LILILOPO ZANZIBAR”

Post a Comment

More to Read