Tuesday, November 10, 2015

HAWA NDIO WACHEZAJI WANAOWANIWA NA VAN GAAL




Kocha Louis Van Gaal wa Manchester United anawania saini za wachezaji ‘mawinga’ wenye kasi zaidi ili kuipa nguvu safu ya ushambuliaji ambayo imekua ikisuasua tangu kuanza kwa msimu huu.

Van Gaal wiki hii alikaririwa akisema wachezaji wake Juan Mata na Jese Lingard hawana kasi na kwamba ni tatizo huku akihitaji wachezaji wenye kasi pembeni ya kiwanja kuzifumua ngome za timu pinzani.

Miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kuwaniwa na kocha huyo ni pamoja na winga wa Leicester City Mahrez, winga Ayoze Pele wa Newcastle United, Saidio Mane wa Southampton na Gareth Bale wa Real Madrid.

Tangu kuondoka kwa winga mwenye kasi Angel Di Maria, Manchester United haina winga mwingine mwenye kasi zaidi kuzikimbiza safu za ulinzi za timu pinzani huku winga Memphis Depay akishindwa kuonesha kile kilichotarajiwa na wengi.

0 Responses to “HAWA NDIO WACHEZAJI WANAOWANIWA NA VAN GAAL”

Post a Comment

More to Read