Tuesday, November 10, 2015
DAVID MOYES ATUPIWA VIRAGO HISPANIA
Do you like this story?
Kocha wa zamani wa vilabu vya Manchester
United na Everton za nchini England, Mscotish David Moyes amefukuzwa kazi rasmi
na klabu ya Real Socieded ya nchini Hispania kutokana na matokeo mabovu ya timu
hiyo.
Moyes ambaye alijiunga na timu hiyo mwezi
October mwaka jana aliisaidia timu hiyo kumaliza ligi ikiwa nafasi ya 12 lakini
hali imekua ni tofauti msimu huu ambao hadi sasa Real Socieded iko katika
hatari ya kushuka daraja kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa katika
nafasi ya 16.
Hatua hiyo imekuja siku kadhaa mara baada ya
kukubali kichapo cha goli 2-0 toka kwa Las Palmas huku wakikabiliwa na mechi
kati ya bingwa mtetezi wa Europa ligi timu ya Sevilla na baadaye mabingwa wa
klabu bingwa Ulaya Barcelona.
Aliyekua kocha msaidizi wa Barcelona ametajwa
kuchukua mikoba iliyoachwa na Moyes.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “DAVID MOYES ATUPIWA VIRAGO HISPANIA”
Post a Comment