Tuesday, November 10, 2015
KUZIONA STARS NA ALGERIA LAZIMA UWE NA KIASI HIKI.
Do you like this story?
Shirikisho la
Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo wa Jumamosi kati
ya Tanzania dhidi ya Algeria utakaochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam bei ya chini kuwa ni shilingi elfu tano (5,000) tu.
Tiketi za
mchezo huo zitaanzwa kuuzwa siku ya ijumaa katika vituo mbalimbali
vinavyotumiwa na TFF kuuzia tiketi, ambapo kiingilio kingine kitakua ni elfu
kumi (10,000) kwa viti vya VIP B & C, huku kiingilio cha elfu tano kikiwa
ni kwa viti vya rangi ya Bluu, Kijani na rangi ya Machungwa.
Wakati huo huo
kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kinachodhamininiwa na bia ya
Kilimanjaro Premium Lager, kinatarajiwa kurejea nyumbani kesho Jumatano mchana
kwa shirika la ndege la Fastjet tayari kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo dhidi
ya Algeria siku ya Jumamosi.
Stars iliyoweka
kambi nchini Afrika Kusini imekua ikifanya mazoezi kila siku katika uwanja wa
Edenvale, ambapo mpaka sasa wachezaji wote wapo katika hali nzuri hakuna
majeruhi na kila mmoja yupo tayari kwa mchezo wa Jumamosi.
Kocha Mkuu wa
Taifa Stars, Charles Mkwasa amesema vijana wake wapo vizuri kifaya, kifikra na
morali ni ya hali juu “wachezaji wamekua wakifanya mazoezi kwa nguvu na
kuonyesha umakini mkubwa” alisema Mkwasa.
Aidha Mkwasa
amewaomba watanzania na wadau wote wa mpira wa miguu nchini kujitokeza kwa
wingi kuwapa sapoti ya kuwashangilia vijana katika mchezo dhidi ya Algeria
Jumamosi, kwani kutawafanya wachezaji kujisikia wapo nyumbani na kucheza kwa
nguvu zaidi.
Wachezaji wa
kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu walioshinda kombe la
Ligi ya Mabingwa mwishoni mwa wiki na klabu yao ya TP Mazembe wanatarajiwa
kuungana na wenzao kambini kesho jijini Dar ess alaam.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KUZIONA STARS NA ALGERIA LAZIMA UWE NA KIASI HIKI.”
Post a Comment