Thursday, November 12, 2015
-LOWASSA KUTOA TAMKO JUMAMOSI BAADA YA KUKOSA URAIS
Do you like this story?
Aliyekuwa
mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
Edward Lowassa, ambaye pia alikuwa akiungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa
Katiba ya Wananchi (Ukawa), anatarajiwa kunguruma jijini Arusha Jumamosi ambapo
atatoa tamko kuhusu uchaguzi mkuu uliopita.
Akizungumza
katika mkutano wa kampeni za ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema,
anayetetea tena nafasi hiyo, alisema Lowassa atazungumza na Watanzania Jumamosi
kupitia wakazi wa Arusha.
Alisema
pamoja na kuja kumnadi yeye katika kinyang’anyiro cha ubunge, Lowassa pia
anatarajiwa kutoa tamko kuhusu uchaguzi mkuu uliopita na namna alivyoibiwa kura
za urais.
“Angetoa
tamko siku ile ya kwanza ya matokeo ya uchaguzi, tungeharibu nchi,” alisema na
kuongeza: “Lowassa alishinda kwa asilimia nyingi kuliko kura alizopata Rais Dk.
John Magufuli, aliyekuwa mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Alisema
nchi imenusurika kutokana na busara za viongozi wa Ukawa kutotoa tamko lolote
wakati huo.
“Atakuja
Jumamosi, hivyo tusubiri tamko kuhusu hatua gani zinachukuliwa…tuwe na subira,”
alisema.
Akizungumzia
uchaguzi wa ubunge unaotarajiwa kufanyika Desemba 13, mwaka huu jijini hapa,
Lema aliwataka wakazi wa jiji hili kutokata tamaa na matokeo ya uchaguzi mkuu
uliopita.
“Hatuna
namna yoyote ile kushindwa kuleta maendeleo jimboni hapa iwapo tumepata
madiwani 24 kati ya kata 25 zilizopo. “Kama tutashindwa kuleta maendeleo hadi
mwaka 2020 huku meya, naibu wake na wenyeviti wa kamati, wote ni wa Chadema,
basi mtupige chini na kuwachagua wengine.
Mapema
Mbunge Mteule wa Jimbo la Mbeya, Joseph Mbilinyi (Chadema), alisema ingawa
wakazi wa Arusha wana hasira kufuatia matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita, lakini
hasira zao haziwezi kuzidi zile za wakazi wa Mbeya.
Alisema
viongozi wao mara zote wametaka kutoa tamko kwa kuzungumza na wananchi, lakini
CCM imekuwa ikikaba hadi penati.
Alisema
katika jimbo lake, wananchi wamewachagua madiwani 26 wa Chadema na kuwaachia
CCM kata tisa, hivyo watapata nafasi nzuri ya kujadili maendeleo katika Baraza
la Madiwani na siyo siasa kama ilivyokuwa awali.
Mbunge
wa Viti Maalum kutoka Kilimanjaro, Lucy Owenya, alisema Lema alifanya kazi
katika mazingira magumu ya halmashauri ambayo ilikuwa ikiongozwa na madiwani wa
CCM.
Alisema
kwa vile wakazi wa Arusha wamewachagua madiwani wa Chadema 24 kati ya 25, Lema
sasa atafanya kazi nzuri ya kuwaletea maendeleo wananchi wake.
Mbunge
Mteule wa Simanjiro, James Ole Millya (Chadema), alisema amefanya kitu kimoja
kikubwa cha kuondolewa bungeni mpiga kelele bungeni.
Alisema
wakifika bungeni, kitu cha kwanza ni kudai Tume Huru ya Uchaguzi, jambo ambalo
alisema bila kuwa na tume hiyo CCM itaendelea kuwaibia kura.
CHANZO: NIPASHE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “-LOWASSA KUTOA TAMKO JUMAMOSI BAADA YA KUKOSA URAIS”
Post a Comment