Monday, November 9, 2015
MASHABIKI LIVERPOOL WAMSIKITISHA KLOPP ANFIELD
Do you like this story?
Baadhi ya mashabiki wa Liverpool jana
walimuacha peke yake kocha wao Jurgen Klopp mara baada ya mlinzi wa Crystal
Palace, Scot Danny kufunga goli la ushindi katika dakika ya 82 ya mchezo na
kufanya matokeo kuwa 2-1.
Hicho ni kipigo cha kwanza kwa kocha Jurgen
Klopp tangu atue Liverpool hivi karibuni kuchukua mikoba ya Brendan Rogders
aliyetupiwa virago mwezi uliopita.
Akielezea tukio hilo mara baada ya mchezo,
kocha huyo raia wa Ujerumani alisema amesikitishwa sana na kitendo hicho cha
mashabiki kumkimbia na kumuacha peke yake wakati timu ikihangaika kurudisha
bao, hali anayoisema kuwa alijihisi mpweke zaidi na kusikitishwa sana na tukio
hilo.
Klopp amewataka mashabiki kuwa wavumilivu na
kwamba haipendezi kutoka uwanjani kabla ya dakika ya mwisho kwani kwenye mpira
lolote linaweza kutokea na kwamba ni vizuri kuisapoti timu hadi mwisho.
Aidha katika tukio jingine, Klopp alishuhudia
kuumia vibaya kwa mlinzi wake wa kati Mamadou Sakho ambaye leo atafanyiwa scan
kuona ni muda gani atakua nje ya uwanja.
Klopp amesema ni heri apoteze mechi hata kwa
bao 3-1 kuliko kumpoteza mchezaji kwa majeruhi, kwani kwake mchezaji ndiye
muhimu zaidi kuliko matokeo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MASHABIKI LIVERPOOL WAMSIKITISHA KLOPP ANFIELD”
Post a Comment