Monday, November 9, 2015
MAWAZIRI SITA WAMEACHA KAZI ZANZIBAR
Do you like this story?
Mawaziri
sita wajiuzulu kutoka katika Chama cha upinzani CUF, mawaziri hao wamechukua
hatua hiyo kutokana na msuguano wa kisiasa visiwani humo.
Waziri
wa sheria na katiba Abubakar Khamis Bakary alitoa kauli hiyo wakati akijibu
maswali ya waandishi wa habari juu ya maazimio yaliyofikiwa na baraza la chama
la Halmashauri kuu ya Taifa.
Mawaziri
wengine waliojiuzulu ni Fatma Abdulhabibu Fereji,Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu
wa Rais wa kwanza, waziri wa Biashara, Viwanda na Makoso Nassor Ahmed Mazrui,
Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Juma Duni Haji, Waziri wa afya Rashidi
Suleiman na Waziri wa Uvuvi na Mifugo Abdillah Jihadi.
Na
wengine ni, Haji Mwandani Makame aliyekuwa Naibu Waziri wa Ardhi na Nyumba,
Maji na Nishati, Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo Zahara Ali Hamed na Naibu
Waziri wa Kilimo Maliasili Mtumwa Kheir Mbarak.
Kwa
mujibu wa Abubakary kila Waziri na Manaibu wao wamekabidhi magari ya serikali
na vifaa vingine kwa mamlaka na kwa mujibu wa kifungu cha sheria cha (28) ya
katiba ya Zanzibar, umiliki wa ofisi kwa ajili ya wote akiwemo na Rais Dr Ali
Mohamed Shein na mawaziri kumalizika Novemba 2.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MAWAZIRI SITA WAMEACHA KAZI ZANZIBAR”
Post a Comment