Monday, November 9, 2015

PICHA ZA RAIS MAGUFULI HOSPITALI YA MUHIMBILI









Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.John Pombe Magufuli leo amefanya ziara nyingine ya kushtukiza katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kujionea hali ya utoaji huduma kwa wagonjwa.

Akiwa hospitalini hapo, Rais Magufuli alipata fursa ya kuongea na wagonjwa.

Awali Rais Magufuli alifika katika Hospitali ya Agha Khan kumjulia hali Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Dk. Hellen Kijo Bisimba anayepatiwa matibabu na vipimo katika hospitali hiyo baada ya jana kupata ajali katika makutano ya barabara ya Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es Salaam.

0 Responses to “ PICHA ZA RAIS MAGUFULI HOSPITALI YA MUHIMBILI ”

Post a Comment

More to Read