Friday, November 6, 2015
MISRI YAZUIA NDEGE ZA SHIRIKA LA UINGEREZA
Do you like this story?
Serikali ya Misri
imesimamisha safari za shirika la ndege la Easyjet ambalo lilikuwa limepangiwa
kuwasafirisha baadhi ya Waingereza waliokwama mji wa Sharm el-Sheikh leo.
Ndege za shirika la Easyjet pamoja na ndege
za mashirika ya Monarch, Thomson na British Airways ndizo zilizokuwa
zimepangiwa kuwasafirisha Waingereza waliokuwa Sharm el-Sheikh baada ya Uingereza
kusitisha safari za ndege za kuingia na kutoka mji wa Sharm el-Sheikh
Jumatano.
Hii ni baada ya kuibuka kwa uwezekano kwamba
huenda ndege ya Urusi iliyoanguka baada ya kupaa kutoka mji huo Jumamosi
iliyopita ikiwa na abiria 224 ililipuliwa.
Maafisa wa Easyjet wamesema maafisa wa Misri
hawakubali ndege za Uingereza zitue katika uwanja huo wa ndege.
Ndege mbili za shirika hilo zilizokuwa
zimepangiwa kuondoka kutoka viwanja vya ndege vya Gatwick na Luton nchini
Uingereza bado zitaondoka kama zilivyopangiwa.
Lakini maafisa wa Easyjet wamesema ndege
nyingine zinazopanga kuondoka kutoka Uingereza kwenza Sharm el-Sheikh
kuwachukua abiria hazitaweza kuhudumu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MISRI YAZUIA NDEGE ZA SHIRIKA LA UINGEREZA ”
Post a Comment