Friday, November 6, 2015
ACT WAZALENDO YAPATA MGOMBEA UBUNGE ARUSHA MJINI
Do you like this story?
Hatimaye Chama cha ACTWazalendo mkoani
Arusha kimempata mgombea atakayepeperusha bendera yake katika uchaguzi mdogo wa
ubunge katika Jimbo la Arusha Mjini.
Hatua hiyo imekuja baada ya chama hicho
kuhaha kwa siku kadhaa hadi dakika za mwisho kumpata mtu wa kuwania jimbo hilo
baada ya uchaguzi kuahirishwa kutokana na kifo cha aliyekuwa mgombea kupitia
chama hicho, Estomih Mallah kufariki dunia katikati ya kampeni.
Katibu wa chama hicho mkoani Arusha,
Daniel Olotu alimtaja Navoy Mollel kuwa ndiye mgombea atakayepeperusha bendera
ya chama hicho baada ya kushinda katika kura za maoni kwa kupata alama 62.
Olotu alisema mkutano mkuu wa chama
hicho ulimpitisha Mollel baada ya kuwashinda wenzake wanane, akifuatiwa na
Hagai Mollel aliyepata kura 34 na John Saitabau aliyepata kura 22.
Uchaguzi huo unafanyika sambamba na
majimbo mengine matatu ya Ulanga Mashariki, Handeni Mjini na Ludewa ambako
wagombea wa CCM walifariki dunia pamoja na Lushoto ambako mgombea wa Chadema
alifariki dunia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ACT WAZALENDO YAPATA MGOMBEA UBUNGE ARUSHA MJINI”
Post a Comment