Friday, November 6, 2015
MASANJA MKANDAMIZAJI NA KUGOMBEA UBUNGE WA LUDEWA
Do you like this story?
Wagombea
tisa akiwemo mdogo wake marehemu Deo Filikunjombe na mchekeshaji Masanja
Mkandamizaji wamejitosa kuwania ubunge wa jimbo la Ludewa,Mkoani Njombe kupitia
tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Uchaguzi wa kumpata Mbunge wa jimbo hilo ulilazimika
kuhairishwa baada ya kutokea kifo cha aliyekuwa mbunge na mgombea ubunge wa
jimbo hilo kupitia CCM, Deogratius Filikunjombe.
Miongoni wa waliojitokeza kwenye kinyang'anyiro hicho ndani
ya CCM ni mdogo wa marehemu, Phillipo Filikunjombe na msanii wa vichekesho na
muimbaji wa nyimbo za Injili Emmanuel Mgaya maarafu kwa jina la 'Masanja
Mkandamizaji'.
Na wagombea wengine ni Johnson Mgimba, James Mgaya, Zephania
Jwahula, Deo Ngalawa, Dk Evaristo Mtitu na Simon Ngatuka.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ MASANJA MKANDAMIZAJI NA KUGOMBEA UBUNGE WA LUDEWA”
Post a Comment