Friday, November 6, 2015

RAIS JOHN MAGUFUL, AMEMUAPISHA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI GEORGE MASAJU




Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ndg George Masaju ameapishwa rasmi asubuhi ya leo na Rais John P. Magufuli.

Uteuzi wa Mwanasheria huyo wa Serikali ulifanyika jana Novemba 5, 2015 mara tu baada ya rais Magufuli kuapishwa baada ya muda wa Serikali ya awamu ya nne kufikia kikomo.

Aidha, baada ya uteuzi kabla ya kumuapisha Masaju, rais huyo wa awamu ya tano ameitisha Bunge tarehe 17 Novemba 2015 na tarehe 19 Nov 2015 ambapo pia anatazamiwa kupendekeza jina la Waziri Mkuu.

0 Responses to “ RAIS JOHN MAGUFUL, AMEMUAPISHA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI GEORGE MASAJU ”

Post a Comment

More to Read