Sunday, December 13, 2015
.MAMLAKA YA MAPATO NCHINI TRA YAPANGA UTARATIBU WA KUTOA MACHINE ZA EFD"S KWA WAFANYA BIASHARA
Do you like this story?
Mamlaka
ya mapato Tanzania TRA inaangalia utaratibu wa kutoa bure mashine za
kutolea risiti za EFD’s kwa wafanyabiashara ili kurahisisha ukusanyaji wa kodi.
Kaimu kamishna
mkuu wa TRA Dr.Philiph Mpango amesema hayo wakati akitoa taarifa kwa
vyombo vya habari ambapo amesema mwisho wa watumishi wa mamlaka hiyo kujaza
fomu za mali wanazomiliki ni December 15 huku akiomba wananchi kusaidia
kufichua vitendo vya ufisadi kweneye mamlaka hiyo.
Kuhusu
waliotorosha makontena bila kulipia ushuru amesema
wafanyabiashara 13 tuu ndio wamemaliza kulipa kwa hiari katika muda
uliotolewa na rais na wengine 15 wamelipa sehemu na bado wanadaiwa na
watalazimika kulipa kwa mabavu ambapo kiasi kilichopatikana ni shilingi
bilioni 10.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)


0 Responses to “.MAMLAKA YA MAPATO NCHINI TRA YAPANGA UTARATIBU WA KUTOA MACHINE ZA EFD"S KWA WAFANYA BIASHARA”
Post a Comment