Wednesday, December 16, 2015
MKUU WA MKOA WA MBEYA ABBAS KANDORO ATOA CHANGAMOTO KWA TCRA
Do you like this story?
NA SAMWEL NDONI, MBEYA
MKUU
wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amelitaka baraza la ushauri la watumiaji wa
huduma za mawasiliano Tanzania (TCRA-CCC), kubuni na kuweka mikakati mizuri
itakayoboresha huduma za mawasiliano ili
kuendana na kasi ya ongezeka la watumiaji wa mawasiliano nchini.
Kandoro
amesema kuwa kumekuwepo na ongezeko la watumiaji wa simu za kiganjani kutoka
watu miliioni 28, mwaka jana hadi kufikia watu milioni 33 mwezi mwachi mwaka huu.
Akizungumza
wakati akizindua semina ya siku moja ya kuelimisha watumiaji wa huduma za
mawasiliano nchini iliyoandaliwa na TCRA-CCC, alisema kuwa baraza hilo lina
wajibu wa kubuni njia na kuweka mikakati ili kutoa huduma kwa watumiaji wa mawasiliano itakakayoendana na ukuaji wa sekta hiyo.
Hata
hivyo aliwataka wanafunzi wa vyuo mbalimbali nchini kutumia teknolojia ya
mawasiliano ya intaneti kwa kujiongezea uelewa ili kuendana na changamoto za
dunia badala ya kutumia kupekua mitandao ya kijamii ambayo haina faida.
Amesema
kuwa ikiwa wanafunzi watutumia vizuri mitandao kwa kujisomea itawajengea uwezo
wa kuelewa mambo mbalimbali na kinyume
na hapo taifa litaendelea kuwa kizazi kisichokuwa na maadili kutokana na
matumizi mabaya ya mtandao.
Mwenyekiti
wa TCRA-CCC, Stanley Mwabulambo alisema semina hiyo imewashirikisha wadau
mbalimbali wa mawasiliano wakiwemo wanafunzi wa vyuo TEKU, Tumaini, MUST, TIA
Mzumbe, wawakilishi kutoka mamlaka ya udhibiti wa nchi kavu na majini Sumatra,
jeshi la polisi, mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA, vikundi, asasi, taasisi na
wadau wengine.
Amesema
kuwa lengo la semina hiyo ni kuelimisha, kuhamasisha na kutambua changamoto za
watumiaji wa mtandao sambamba na kuelimisha watumiaji hao juu ya matumizi
sahihi ya mtandao.
MWISHO
.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)

0 Responses to “MKUU WA MKOA WA MBEYA ABBAS KANDORO ATOA CHANGAMOTO KWA TCRA”
Post a Comment