Wednesday, December 16, 2015
MWANAFUNZI WA UDSM AUAWA KWA RISASI
Do you like this story?
![]() |
| Mwanafunzi wa UDSM, Mutaengerwa Mafwiri enzi za uhai wake. |
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM), Mutaengerwa Mafwiri ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa
kuwa majambazi jana usiku eneo la Msewe jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwa njia ya simu, Kamanda wa
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Camillus Wambura amekiri kutokea
kwa tukio hilo.
Kwa mujibu wa Kamanda Wambura tukio hilo
lilitokea jana usiku majira ya saa mbili baada ya watu wanaosadikiwa kuwa
majambazi kuvamia duka moja lililopo maeneo hayo na kupora simu, vocha na fedha
taslimu kiasi cha shilingi 100,000/=.
Wakati wakiondoka eneo la tukio wananchi
walianza kuwapigia kelele ndipo walipoanza kupiga risasi ovyo ambapo mojawapo
ilimpata Mafwiri aliyekuwa katika banda la chipsi na kumsababishia umauti.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili na uchunguzi bado unaendelea.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)



0 Responses to “ MWANAFUNZI WA UDSM AUAWA KWA RISASI”
Post a Comment