Wednesday, December 23, 2015
SOMALIA YAPIGA MARUFUKU SIKUKUU YA KRISMASI
Do you like this story?
Serikali ya Somalia imepiga marufuku sherehe
za kuadhimisha Sikukuu ya Krismasi katika mji mkuu wa Mogadishu.
Mkurugenzi mkuu katika wizara ya masuala ya
dini, Sheikh Mohamed Khayrow, ameonya kuwa maadhimisho kama hayo
yasiyofungamana na dini ya Kiislamu yanaweza kusababisha mashambulizi kutoka
kundi la wanamgambo wa Al Shabab.
“Maofisa wote wa kulinda usalama wanapaswa
kusimamisha ama kuvunja mikutano ya aina yoyote yenye nia ya kuadhimisha
sikukuu hiyo isiyofungamana na dini ya Kiislamu.” alisema Sheikh Mohamed
Mwaka uliopita wapiganaji wa Al shabab
walishambulia kambi ya majeshi ya muungano wa Afrika (AU) iliyopo Mogadishu
wakati wanajeshi hao walikuwa wakisherehekea sikukuu ya Krismasi.
Wanajeshi 5 waliuawa katika shambulizi hilo
la kuvizia.
Asilimia kubwa ya raia wa Somalia ni
wasilamu.
Credit: BBC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)


0 Responses to “SOMALIA YAPIGA MARUFUKU SIKUKUU YA KRISMASI”
Post a Comment