Wednesday, December 23, 2015
WAZIRI AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI WA HOSPITALI YA OCEAN ROAD
Do you like this story?
WAZIRI wa
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto amemsimamisha kazi
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dk.Diwani Msemo ili
kupisha uchunguzi pamoja na mambo mengine ili kubaini mgongano wa
kimaslahi ulioathiri utendaji wa taasisi hiyo chini ya kaimu mkurugenzi
huyo.
Kwa mujibu wa
taarifa iliyotolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na
Watoto mwenye Wizara hiyo, Ummy Mwalimu imesema kuwa kutokana na ziara
alizofanya Rais Dk. John Pombe Magufuli inaonyesha kukosekana kwa dawa katika
hospitali za Serikali huku vituo vya afya vya binafsi vikiwa na dawa.
Taarifa ya
Waziri huyo imesema kuwa upungufu wa dawa umeendelea kujitokeza kwa karibu
zaidi na baadhi ya wagonjwa walieleza kwa uchungu jinsi wanavyopata dawa kwa
tabu hatazile wanazotakiwa wapate kwa bei ya ruzuku au zilezinazotakiwa
kutolewa bure na serikali.
Kwa msingi wa
uwazi na uwajibikaji ameagiza watendaji wote wa sekta ya afya hususani wakuu wa
vituo vya kutolea huduma za afya, Wafamasia, Wauguzi na Waganga Wafawidhi wa
vituo vya kutolea huduma za afya kukiri kwa maandishi kwa ngazi zao za
uwajibikaji endapo wanamiliki Hospitali, Zahanati, Kiliniki, Maduka ya Dawa
ndani ya siku 21 kuanzia leo Desemba 23 mwaka huu ambapo agizo hilo
limeotolewa.
Aidha taarifa
hiyo imedai kuwa kufanya hivyo kutaziba mianya ya upotevu wa dawa na vifaa tiba
katika vituo vya umma.
Bodi ya Taasisi
ya Ocean Road imeagizwa kutafuta mtu atakayekaimu nafasi iliyoachwa wazi na
Dk.Msemo anayefanyiwa uchunguzi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)


0 Responses to “WAZIRI AMSIMAMISHA KAZI MKURUGENZI WA HOSPITALI YA OCEAN ROAD”
Post a Comment