Wednesday, December 23, 2015
MAGUFULI KUOMBEWA UINGEREZA
Do you like this story?
Na Gabriel Ng’osha
KASI ya Rais John Pombe Magufuli ‘JPM’ inazidi kuwashangaza wengi ambapo wachungaji wa Kanisa la Calvary Charismatic Baptist Church Swahili Service la jijini London, Uingereza wameamua kumfanyia maombi maalumu Jumatatu ijayo.

Maombi hayo yamepangwa kufanyika katika
kanisa hilo lililopo 119 East India, Dock Road Poplar London EI46DE, huku mgeni
rasmi akitarajiwa kuwa Naibu Balozi wa Tanzania nchini humo, Msafiri Marwa na
yataongozwa na kiongozi mkuu wa kanisa hilo, Bob Baraka, Loise Gitahi na Askofu
Francis Sarpong sambamba na wahamasishaji Joe Matonda na Teddy Mpangala ambao
wamewaomba Waafrika wajitokeze kwa wingi siku hiyo.
Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa
wahamasishaji wa tamasha hilo ambaye ni mfanyabiashara wa Kitanzania nchini
humo, Chris Lukosi alisema kasi ya utendaji wa kiongozi huyo wa Tanzania
imewavutia Waafrika wengi wanaoishi Uingereza.
“Rais amekuwa gumzo kila kona, Waafrika na
wasomi wanaoishi nje wanamkubali na kutamani kuona Bara la Afrika likipata
viongozi kama yeye,” alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)

0 Responses to “ MAGUFULI KUOMBEWA UINGEREZA”
Post a Comment