Tuesday, January 5, 2016
KERR KAWACHANA LIVE WACHEZAJI WANAOZINGUA
Do you like this story?
Kocha mkuu wa Simba Dylan Kerr amewaangushia
zigo la lawama wachezaji wake ambao ‘walizingua’ kwenye mchezo wao kwanza wa
kundi A wakati wakicheza dhidi ya Jamhuri kutoka Pemba.
Kerr amesema anashangazwa na wachezaji wake
kushindwa kupasia kamba wakati wanapobaki wao na golikipa kitu ambacho wamekuwa
wakihifanyia kazi kila kukicha wanapokuwa kwenye mazoezi. Kerr hakusita kumtaja
mshambuliaji wa kimataifa Paul Kiongera kutoka Kenya pamoja na mchezaji wa Azam
Joseph Kimwaga anayecheza kwa mkopo Simba kuwa ndio wamemuangusha kwenye mchezo
wa jana usiku.
“Kabla hatujafunga goli la kwanza tulipoteza
nafasi nne. Joseph Kimwaga alipoteza nafasi mbili za wazi, Kiongera alikosa
goli akiwa umbali wa mita tatu kutoka golini, tumemsajili mchezaji huyu kutoka
Kenya ambaye anatakiwa kuwa mshambuliaji wa kiwango cha dunia lakini anashindwa
kufunga goli akiwa mita tatu kutoka golini. Kimwaga ameshindwa kufunga ndani ya
mita sita lakini ni vitu ambavyo tunafanya kila siku kwenye mazoezi”, alilalama
kocha huyo.
“Sijali watu wanasema nini au wanafikiria
nini, wachezaji wangu wengi wamecheza zaidi ya mechi 20 ukijumlisha na mechi za
timu ya taifa wengine wamecheza zaidi ya mechi 29 achilia mbali mechi za
kirafiki za pre season. Kwahiyo haya mashsindano tunawaachia wachezaji ambao
hawajapata nafasi ya kucheza ili waoneshe uwezo wao”.
“Hii ni fursa kwao kunishawishi niwape nafasi
kwenye kikosi cha kwanza wanatakiwa kuwa na njaa, lakini naona bado wanahitaji
muda zaidi. Naogopa kuwatumia wachezaji wa kikosi cha kwanza kwasababu ni
hatari sana wanaweza kupata majeraha ikiwa shida kwenye ligi. Kwamfano, Hassan
Kessy ni majeruhi kwahiyo kumchezesha Emery ni ku-risk endapo akipata majeruhi
timu itakuwa imepoteza wachezaji muhimu wa nafasi moja”.
“Kama kocha, huu ni wakati muafaka kutafuta
wachezaji mbadala endapo wachezaji wengine watakosekana kwenye kikosi cha
kwanza kutokana na kupewa kadi, majeruhi au wakiwa wagonjwa. Kwahiyo kwa upande
wangu mashindano haya nimeamua kuwapa nafasi wachezaji ambao hawapati nafasi ya
kucheza mara kwa mara”.
Licha ya kulazimishwa sare ya kufungana kwa
magoli 2-2 na Jamhuri, kikosi cha Simba kilipoteza nafasi nyingi za kufunga za
wazi kitu ambacho kimemkasirisha kocha wa mnyama na kuamua kuwachana live
wachezaji wanaozingua.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)


0 Responses to “KERR KAWACHANA LIVE WACHEZAJI WANAOZINGUA”
Post a Comment