Tuesday, January 5, 2016
FELLAINI KUONDOKA MAN UNITED MWEZI HUU?
Do you like this story?
Imeelezwa kuwa klabu ya Manchester United
haina mpango wa kumuachia kiungo wao raia wa Ubelgiji, Maruane Fellaini katika
dirisha hili dogo la usajili (January Transfer Window) pamoja na kutakiwa kwa
mchezaji huyo na vilabu mbalimbali barani Ulaya.
Gazeti la Daily Mail la nchini Uingereza
limeripoti kuwa tayari klabu ya soka ya Manchester United imeitolea nje ofa ya
AC Milan ya Italia inayomhitaji kiungo huyo kwa mkopo mwezi huu.
Gazeti hilo limeandika kuwa Maruane Fellaini
yuko tayari kupigania nafasi yake kikosini hapo huku pia akiamini kuwa future
yake imelalia Old Trafford pamoja na kuhitajika na vilabu mbalimbali hivi sasa.
Maruane Fellaini alianza mara nane tu msimu
huu huku akiwa miongoni mwa kikosi kilichopokea vichapo vinne mfululizo, lakini
hajacheza katika mechi mbili za mwisho dhidi ya Chelsea na Swansea na
kushuhudia United ikikusanya alama nne katika michezo hiyo miwili.
Habari nyingine za usajili kikosini hapo
zinasema kuwa kiungo Nick Powell anatakiwa kwa mkopo na klabu ya soka ya
Championship ya Preston City mwezi huu wa Januari.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)


0 Responses to “FELLAINI KUONDOKA MAN UNITED MWEZI HUU?”
Post a Comment