Tuesday, January 5, 2016

WAAFRIKA TUMEJALIWA SANA MIPANGO, HEBU CHEKI PLAN ZA CECAFA MWAKA 2016


Kutoka kulia: Habimona Aimable, Abdiqani Said Arab, Rais wa CECAFA Mutasim Gafaar, Katibu Mkuu Nicholas Musonye na Souleiman Hassan Wabri wakiwa kwenye mkutano Khartoum Jumatatu Jan 4 2016
Kutoka kulia: Habimona Aimable, Abdiqani Said Arab, Rais wa CECAFA Mutasim Gafaar, Katibu Mkuu Nicholas Musonye na Souleiman Hassan Wabri wakiwa kwenye mkutano Khartoum Jumatatu Jan 4 2016


Shirikisho la vyama vya soka vya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limetangaza programs ambazo zitasaidia kukuza soka la nchi za ukanda huo.

Kikao cha kwanza cha bodi tangu kufanyika kwa uchaguzi kilichoongozwa na rais wa CECAFA Dr. Mutasim Gafaar  kwenye mji wa Khartoum kimefikia maadhimio kadhaa, kamati kuu imepitisha mikakati mipya ambayo imebeba mipango ya program za maendeleo.

Michuano miwili ya U-17 kwa wanaume na wanawake itafanyika mwaka 2016 kama inavyooneshwa kwenye mipango mipya iliyopitishwa na shirikisho linalosimamia soka la Afrika.

Mikakati mingine ya maendeleo ambayo utekelezaji wake utaanza mwaka 2016 ni mafunzo kwa makocha, waamuzi, beach soccer (soka la mchangani) pamoja na mafunzo ya utawala kwa ajili ya kujenga nguvu ya CECAFA.

CECAFA ambayo ndiyo chama cha soka chenye michuano mikongwe Afrika kimedhamiria kuongeza nguvu yake kwenye soka na kuwavutia wawekezaji kwa kuboresha mashindano pamoja na mambo mengine ya kimaendeleo.

“Kamati kuu inatambua uhitaji na umuhimu wa wadhamini na kwasababu hiyo, tumeamua kutafuta wadhamini kwa ajili ya michuano yetu”, alisema makamu wa rais wa CECAFA Abdiqani Said Arab baada ya kikao cha kamati kuu.

Alisema pia, shirikisho hilo litaimarisha uhusiano na ushirikiano na vyama pamoja na mashirikisho mengine ya soka ulimwenguni.

Kama mipango na mikakati hiyo itafanikiwa kutekelezwa, huo utakuwa ni mwanzo wa kutimia kwa ndoto za CECAFA za muda mrefu lakini pia utakuwa ni mwanzo mzuri kwa uongozi uliochaguliwa chini ya Dr. Mutasim Gafaar wa Sudan.

0 Responses to “WAAFRIKA TUMEJALIWA SANA MIPANGO, HEBU CHEKI PLAN ZA CECAFA MWAKA 2016”

Post a Comment

More to Read