Thursday, March 31, 2016
WANANCHI WAANZA KUGOMBANIA KITI ALICHOKIKALIA RAIS MAGUFULI KWENYE MGAHAWA JIJINI MWANZA.
Do you like this story?
Mgahawa
aliotumia Rais John Magufuli kupata mlo wa mchana na msafara wake juzi kwenye
Uwanja wa Ndege wa Mwanza, umekuwa kivutio kwa wateja wengi wakinunua chakula
na kutaka kukalia kiti na meza alivyotumia kiongozi huyo.
Meneja wa
mghahawa huo wa Victoria, Elizabeth Maneno (pichani) alisema jana kwamba hali
hiyo ilijitokeza mara baada ya Rais kuondoka hapo.
“Hata
leo tumepokea wateja wengi kulinganisha na siku nyingine, baadhi yao wanaagiza chakula kwa sharti la
kutaka kukikalia kiti na meza aliyotumia Rais Magufuli,” alisema
Elizabeth.
Akizungumzia
hali ilivyokuwa juzi kabla na wakati wa ugeni huo meneja huyo alisema: “Ilikuwa
ni hofu na woga uliochanganyika na furaha kumwona Rais akiingia kwenye mgahawa
wetu wa chai ya rangi ya Sh200 na ya maziwa Sh300.
“Mshtuko
wetu uligeuka furaha baada ya kubaini kuwa oda ya sahani 28 za kubeba
(takeaway), tulizoagizwa mapema asubuhi bila kuelezwa zinakoenda zilikuwa za
ujumbe wa Rais,” alisema na kuongeza:
“Kabla
Rais Magufuli hajaingia kwenye mgahawa wetu, alikuja mtu mmoja tusiyemfahamu na
kuagiza sahani 28 za chakula kwa gharama ya Sh5,000 kila moja,”
Alisema baada
ya kumtaarifu mteja wake kuwa chakula kiko tayari, alielekezwa kuandaa meza na
viti kwa sababu wageni wake (wa mteja), sasa wameamua kula palepale mgahawani.
“Ghafla
tulimwona Rais anaingia ndani ya mghahawa wetu; kwanza tulishikwa hofu, woga na
kihoro tusijue tufanye nini hadi tulipogutushwa na aliyetoa oda kwa kutuagiza
tugawe chakula alichoagiza,”
alisema meneja huyo; “hapo ndipo tulipobaini kumbe chakula kile kilikuwa cha
ugeni wa Rais.”
Pamoja na chai
ya rangi na ya maziwa, mghahawa huo pia unauza vyakula vya aina mbalimbali kwa
bei kati ya Sh1,500 hadi Sh5,000 kwa vyakula vya kubeba, huku soda ikiuzwa kwa
Sh500 kwa chupa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WANANCHI WAANZA KUGOMBANIA KITI ALICHOKIKALIA RAIS MAGUFULI KWENYE MGAHAWA JIJINI MWANZA.”
Post a Comment