Thursday, March 31, 2016
WAZIRI WA RWANDA AFIA GEREZANI BURUNDI
Do you like this story?
Bujumbura, Burundi
WAZIRI wa zamani wa Rwanda, Jacques Bihozagara
amefariki katika gereza moja nchini Burundi miezi minne baada ya kukamatwa kwa
tuhuma za kufanya ujasusi.
Rwanda
imesema marehemu Jacques alikuwa ameshikiliwa kinyume cha sheria. Balozi wa
Rwanda nchini Ubelgiji ameandika na kusema kifo cha Jacques ni “mauaji”.
Wafungwa
katika gereza alipokuwa ameshikiliwa wanasema alionekana akiwa katika hali
nzuri na kwamba alifariki dakika chache baada ya kuchukuliwa kutoka gereza
kupelekwa hospitali baada ya kuugua.
Umoja
wa Mataifa umekuwa ukiishutumu Rwanda kwa kujaribu kuipindua serikali ya Rais
wa Burundi Pierre Nkurunziza, madai ambayo Rwanda imekuwa ikiyakanusha.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ WAZIRI WA RWANDA AFIA GEREZANI BURUNDI”
Post a Comment