Thursday, June 30, 2016
POLISI YAUA MAJAMBAZI WATATU WALIKUWA WAMEJIFICHA KATIKA MAPANGO YA AMBONI.
Do you like this story?
POLISI mkoani
Tanga imewaua watu watatu katika mapigano ya risasi wanaodaiwa kuhusika katika
mauaji ya watu jijini humo wakiwamo watu wanane waliochinjwa katika Kitongoji
cha Kibatini, Kata ya Mzizima.
Limewahakikishia
wananchi kwamba eneo la Amboni yakiwemo Mapango ya Majimoto yanayodaiwa
kutumiwa na wahalifu waliosababisha mauaji hasa ya wakazi wanane wa Kibatini
lipo salama, baada ya watuhumiwa wengine watatu na silaha mbalimbali kukamatwa
juzi.
Waliokamatwa ni
Abdulkarim Singano, Seif Jumanne na Ramadhani Mohamed ambao baadaye walikufa
kutokana na majeraha ya risasi wakati wa mapigano katika msitu wa Kibatini
wakati askari wakijaribu kuwadhibiti, siku moja baada ya Abuu Seif anayedaiwa
kuwa kiongozi wao kuuawa jijini Dar es Salaam.
Silaha
zilizokamatwa ni bunduki mbili aina ya SMG, bastola moja, risasi 30, mapanga,
majambia ambavyo vimepatikana kupitia msako ulioshirikisha kikosi kazi cha
vyombo vya ulinzi na usalama vilivyohusisha askari kutoka majeshi yote.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paulo alibainisha hayo wakati akitoa taarifa
ofisini kwake jana kwamba, wahalifu hao walikamatwa Juni 28, mwaka huu wakati
askari walipokuwa katika harakati za kuwakamata kwenye msitu wa Kibatini jirani
na mapango ya Majimoto, Kata ya Mzizima jijini Tanga.
“Majambazi
waliohusika kuua wananchi wanane pale Kibatini ndio tumewakamata lakini kwa
bahati mbaya watatu kati yao wamekufa wakati wakidhibitiwa na askari,” alisema Kamanda Paulo.
Alisisitiza wameyakagua yaliyokuwa maficho yao na kujiridhisha kuwa Amboni iko salama na imedhibitiwa.
Alisisitiza wameyakagua yaliyokuwa maficho yao na kujiridhisha kuwa Amboni iko salama na imedhibitiwa.
Mapema wiki
hii, Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, walitangaza kumuua Abuu Seif
aliyeshiriki katika mauaji ya Tanga, baada ya kumpiga risasi alipokataa
kujisalimisha baada ya kubainika kujificha katika nyumba moja jijini Dar es
Salaam. Alifariki dunia akipelekwa hospitali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ POLISI YAUA MAJAMBAZI WATATU WALIKUWA WAMEJIFICHA KATIKA MAPANGO YA AMBONI.”
Post a Comment