Friday, October 7, 2016
ANTONIO GUTERREZ ATEULIWA KUWA KATIBU MKUU MPYA WA UMOJA WA MATAIFA
Do you like this story?
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa
kwa wingi wa kura limemteua aliyekuwa waziri mkuu wa Ureno Antonio Guterres
kuwa katibu mkuu mpya wa umoja huo.
Mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa
unatarajiwa kufanyika wiki ijayo kuidhinisha uchaguzi wake kwa muhula wa miaka
mitano.
Bwana Guterres, mwenye umri wa miaka
67,ambaye aliongoza kitengo cha wakimbizi katika Umoja wa Mataifa kwa kipindi
cha miaka 10 atachukua mahala pake Ban Ki-moon mapema mwaka ujao.
Bwana Ban mwenye umri wa miaka 72,
alimtaja bwana Guterres kama 'chaguo zuri' la kumrithi. "Uzoefu wake kama
waziri wa Ureno, ujuzi wake wa maswala tofauti duniani na ukakamavu wake
utamsaidia katika kuliongoza shirika hilo la Umoja wa Mataifa katika kipindi
muhimu," Ban aliwaambia wanahabari alipozuru mjini Rom.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ANTONIO GUTERREZ ATEULIWA KUWA KATIBU MKUU MPYA WA UMOJA WA MATAIFA”
Post a Comment